MAELEKEZO YA KUTENGENEZA ICING SUGAR Nyumbani -Kwa maelekezo ya picha tafadhali bonyeza hapa Bonyeza hapa , utaona zote na utaelewa vizuri. 1. Chukua sukari yako nyeupe weka kwenye blender au food processor. 2.Washa blender, blend sukari uhakikishe una stop kwa kila sekunde 5 huku ukiangalia kama sukari imeshasagika kuwa unga vizuri. 3.Utakapoona sukari yako imesagika vizuri, weka kijiko kimoja tu cha unga wa mahindi kwenye sukari then blend mara moja tu ichanganyike vzri NOTE: Icing sugar yako tayari kwa matumizi, waweza hifadhi kwenye container ya mfuniko. Note: Unga wa mahindi unasaidia sukari isitengeneze mabuja pale unapohifadhi. MUHIMU: Ukihitaji kutumia icing sugar kwenye keki chota kiasi unachotaka, weka kwa bakuli kisha miminia maziwa fresh au limao kidogo kisha koroga vizuri iwe na uzito wa uji, yani maji yasizidi icing sugar. Hapo itakua tayari kwenye kupambia keki au sconzi. PIA NITAWEKA SOMO LA KUCHANGANYA MAZIWA/JUICE KWENYE ICING SUGAR