JINSI YA KUPIKA VISHETI/VIKOKOTO~Lugha Swahili
Maelekezo ya Picha zote hatua kwa hatua bonyeza hapa
Maelekezo ya Picha zote hatua kwa hatua bonyeza hapa
MAHITAJI
-Unga nagno Kilo 1 na 1/2
-Siagi iliyoyeyushwa Vijiko 2 vya chakula
-1/4 lita ya maziwa au 1/4 kikombe ya maji
-Chumvi kiduchu
-Lita 1 au 1/2 lita ya Mafuta ya kupikia
-Unga nagno Kilo 1 na 1/2
-Siagi iliyoyeyushwa Vijiko 2 vya chakula
-1/4 lita ya maziwa au 1/4 kikombe ya maji
-Chumvi kiduchu
-Lita 1 au 1/2 lita ya Mafuta ya kupikia
MAHITAJI YA SYRUP(SHIRA NYEUPE) YA KUCHANGANYIA KWENYE VISHETI
-Maji kikombe 1
-Sukari nusu na robo
-KIfuniko 1 cha Vanilla
-Hiliki pinje kama 10
-Maji kikombe 1
-Sukari nusu na robo
-KIfuniko 1 cha Vanilla
-Hiliki pinje kama 10
JINSI YA KUANDAA VISHETI
1.Yeyusha siagi.Tia unga wa ngano kwenye bakuli kubwa,kisha tia siagi iliyoyeyushwa
1.Yeyusha siagi.Tia unga wa ngano kwenye bakuli kubwa,kisha tia siagi iliyoyeyushwa
2.Mimina maziwa baridi kidogo kidogo kwenye unga hlf changanya(waweza tumia maji baridi pia)
3.Anza kuchanganya changanya unga na maziwa baridi mpaka utengeneze donge kama la chapati(Usikande ila changanya kawaida)
4.Gawanya donge la unga kwenye madonge matatu3,Sukuma donge moja moja kwa shape ya chapati nene, kisha tumia kisu kukata chapati kwa urefu (Angalia picha kwenye blog jinsi ya kukata).
5.Baada ya kukata kwa urefu, malizia kukata kwa shape ya visheti kama inavoonekana kwenya picha
KAANGA VISHETI VYAKO
-Weka mafuta ya kupikia kwenye karai, acha yachemke, kisha tia vipande vyako vya visheti kwenye mafuta ya moto,weka vipande vichache visibanane sana.
-Weka mafuta ya kupikia kwenye karai, acha yachemke, kisha tia vipande vyako vya visheti kwenye mafuta ya moto,weka vipande vichache visibanane sana.
-Baada ya dk 5 geuza visheti, kaanga upande wa pili mpaka viwe brown.Then,toa visheti weka kwenye chombo kinachochujisha mafuta.
ANDAA SHIRA NYEUPE/SUGAR SYRUP
-Chukua sufuria kubwa, weka sukari, maji na vanilla na hiliki.
-Chukua sufuria kubwa, weka sukari, maji na vanilla na hiliki.
-Acha mchanganyiko uchemke kwenye moto mdogo mpka sukari iyeyuke kabisa, Acha ichemke hadi iwe nzito.
-Shira nyeupe tayari, basi chukua visheti vyako ulivyokaanga changanya kwenye shira ikiwa bado yamoto, koroga koroga hadi visheti vikolee, waweza changanya visheti kidogo kidogo ili shira ishike vizuri.
NB: Hakikisha shira haipoi, ikipoa iweke kwenye moto kidogo ndo uendelee kuchanganyia kwenye visheti.
NB: Hakikisha shira haipoi, ikipoa iweke kwenye moto kidogo ndo uedelee kuchanganyia kwenye visheti.
EPUA VISHETI, VIKISHAPOA VIPO TAYARI KULIWA AU HIFADHI KWENYE CONTAINER KWA MATUMIZI YA BADAE AU BIASHARA
Ma shaa Allah shukran
ReplyDeleteJazakillahu khaira habiibty
ReplyDeleteAty lazima utumie sukari nyeupe..wat abt brown sugar
ReplyDelete