Skip to main content

Pilau la nyama ya ng'ombe



Njoo ujifunze kupika pilau tamu la nyama
  Bonyeza hapa Kupata maelekezo ya picha hatua kwa hatua.

Mahitaji:
-Mchele kilo moja
-Nyama ya ng'ombe iliyochemshwa kg 1
-kitunguu swaumu punje 4-7
-tangaizi kijiko kimoja cha chai
-Kitunguu kikubwa 1
-Mafuta ya kupikia robo kikombe
-nyanya ndogo 3
-Maji vikombe 6 vya chai
-Chumvi
-beef masala kijiko kimoja cha chakula
-Pilau masala vijiko viwili vya chakula
-Viazi vinne vidogo
-Hiliki punje 3 kama wapenda
-njegere zilizochemshwa nusu kikombe cha chai

Maelekezo.
-Kata nyama,osha na uchemsha nyama yako na chumvi kidogo,ukipenda weka tangawizi kidogo.
-Menya vitunguu swaumu na tangawizi twanga, weka pembeni,Chambua mchele weka pembeni.
-Nyama ikishaiva,anza kupika.

Mapishi ya Pilau
-Weka sufuria kwenye moto,weka mafuta,tia vitunguu maji vilivyokatwa, koroga acha viwe brown kidogo,kisha weka vitunguu swaumu na tangawizi iliyopondwa, na beef masala.
-Koroga mpka viwe brown,weka nyanya zilizokatwa,ziache ziive uku ukiwa unakoroga nyanya had zipondeke.
-Nyanya zikisha pondeka ongeza viungo vya pilau,weka na nyama iliyochemshwa koroga.
-nyama ikikolea viungo,weka maji kulingana na mchele wako acha maji yachemke,ongeza chumvi ya kukutosha.
-Osha mchele,tumbukiza kwenye maji yaliyochemka,ongeza viazi,weka njegere zilizo chemshwa,angalia wingi wa maji unatakiwa uone mchele sio ufunike kabsa mchele, kama ni mengi sana punguzia pembeni.
-Punguza moto kama unapikia gesi funikia kwa moto mdogo sana.
-Kama unapikia mkaa,punguza mkaa unaowaka jikoni weka juu ya mfuniko,acha jikoni mkaa kama minne midogo,acha pilau iive kwa dk15-20.
-Baada ya dk 15 funua, geuza pilau angalia kama limeiva,kama bado una kiini ongeza maji ya moto au vuguvugu,hlf endelea kufunikia.
Pilau lako litakuwa tayari,waweza kulila na kachumbari au salad yoyote.

NB:   Bonyeza hapa Kupata maelekezo ya picha hatua kwa hatua.

KUMBUKA KADRI UNAVOJIFUNZA KILA MARA NDIO UNAPOZOEA VIPIMO VYA MAJI, NA MCHELE.SO PRACTISE,PRACTISE UTAJUA TU.

Comments

Popular posts from this blog

NJIA RAHISI YA KUTENGENEZA KEKI YA VANILLA

Jinsi ya Kupika Visheti/Vikokoto~Crunchy Visheti

Half Cake za maziwa