Skip to main content

NJIA RAHISI YA KUTENGENEZA KEKI YA VANILLA



NJIA RAHISI YA KUTENGENEZA KEKI YA VANILLA

-Fuatilia maelekezo ya picha zote bonyeza hapa


MAHITAJI
-Unga wa Ngano Vikombe 2
-Baking powder 1/2 kijiko cha chai
-Baking soda 1/2 kijiko cha chai
-Sukari kikombe 1
-Siagi kikombe 1 kidogo
-mayai 2
-Vanilla vijiko 2 vya chai
-Maziwa fresh kikombe 1 au tumia fanta soda nusu kikombe
-Chumvi kidogo ukipenda(siagi ina chumvi kwa hyo kiduchu)

MAELEKEZO YA JINSI YA KUTENGENEZA KEKI
1.  kwenye bakuli kubwa,Chuja Unga,weka baking poda,weka baking soda, weka chumvi kidogo kisha weka pembeni.

2.Blend sukari yako na blender au twanga sukari kidogo kidogo kufanya sukari iwe kama unga.

3.Kwenye bakuli nyingine, weka siagi na sukari uliyoponda ipige pige  na  mwiko mpaka siagi iwe smooth, kuelekea kama rangi nyeupe hivi(fanya kwa dk10 hv)

4.Baada ya hapo, piga mayai tia kwenye mchanganyiko wa siagi na sukari, kisha weka maziwa au fanta kidogo kidogo.

5.Sasa, chukua ule unga ulioandaa kwenye step ya 1, mimina kidogo kidogo kwenye mix ya mayai,siagi, sukari na maziwa.

6.Koroga mchanganyiko wako mpaka uwe kama uji mzito, koroga kwa kutumia mixer ya mkono au mixer ya umeme.(Angalia kwenye picha)

JINSI YA KUOKA KEKI
-Andaa sufuria ya kuokea paka siagi chini

-Mimina mchanganyiko wako wa uji ukieneza kwenye angle zote za sufuria.

-Kama unatumia oven weka moto mdogo wa 350F

-Kama unatumia mkaa, basi hakikisha umeshawasha mkaa umekolea vizuri, Chukua mfuniko weka makaa ya moto juu ya mfuniko, bakisha mkaa kidogo sana,kisha weka sufuria yenye uji wa keki weka jikoni, funikia na mfuniko wenye makaa.

-Baada ya dk 15-30 utaskia harufu ya kuiva, funua mfuniko chomeka toothpick kwenye keki kuona kama imeiva toothpick ikitoka kavu bas keki imeiva epua.

-Weka kwenye sahani keki yako waweza kata vipande unavyotaka, tayari kuliwa.

NB: Usitumia baking soda au baking poda zilizokaa sana dukani au nyumbani mwisho miezi 6.
-Vifaa vyote vya keki vinapatikana ukihitaji njoo inbox.

Comments

Popular posts from this blog

Jinsi ya Kupika Visheti/Vikokoto~Crunchy Visheti

Half Cake za maziwa