MAELEKEZO YA
KUTENGENEZA ICING SUGAR Nyumbani
-Kwa maelekezo ya
picha tafadhali bonyeza hapaBonyeza hapa , utaona zote na utaelewa vizuri.
1. Chukua sukari yako
nyeupe weka kwenye blender au food processor.
2.Washa blender, blend
sukari uhakikishe una stop kwa kila sekunde 5 huku ukiangalia kama sukari
imeshasagika kuwa unga vizuri.
3.Utakapoona sukari
yako imesagika vizuri, weka kijiko kimoja tu cha unga wa mahindi kwenye sukari
then blend mara moja tu ichanganyike vzri
NOTE: Icing sugar yako
tayari kwa matumizi, waweza hifadhi kwenye container ya mfuniko.
Note: Unga wa mahindi
unasaidia sukari isitengeneze mabuja pale unapohifadhi.
MUHIMU: Ukihitaji
kutumia icing sugar kwenye keki chota kiasi unachotaka, weka kwa bakuli kisha
miminia maziwa fresh au limao kidogo kisha koroga vizuri iwe na uzito wa uji,
yani maji yasizidi icing sugar. Hapo itakua tayari kwenye kupambia keki au
sconzi.
PIA NITAWEKA SOMO LA
KUCHANGANYA MAZIWA/JUICE KWENYE ICING SUGAR KWA AJILI YA MATUMIZI YA KUPAMBA
KEKI. KAENI TAYARI
safi
ReplyDelete