Mahitaji
1. Unga
wa Ngano-1 kg
2. Mafuta
ya kupikia ya vuguvugu kwa ajili ya kukandia ½ kikombe na ¼ kikombe kwa ajili ya
kuchomea
3. Chumvi
kijiko cha chakula 1
4. Sukari
Vijiko 3 vya chakula
5. Maziwa
ya vuguvugu au waweza tumia maji ya vuguvugu
Vifaa
i.
Ubao wa kusukumia chapati na mpini wake
ii.
Frying pan flat na Mwiko wa kugeuzia chapati
iii.
Bakuli kubwa kwa ajili ya kukandia unga
iv.
Sehemu safi flat kwa ajili ya kukandia unga
Instructions/Maelekezo
1. Mimina
Unga kwenye bakuli ya kukandia, mimina chumvi, mimina sukari pia kasha changanya
vizuri.
2. Mimina
mafuta ya vuguvugu kwenye bakuli ya unga halafu changanya vizuri kuondoa crumps
3. Anza
kumimina maziwa ya vuguvugu kidogokidogo, kwenye unga huku ukiwa una changanya
unga na maziwa ushike vizuri, mimina maziwa mpaka pale unga utakapokuwa tayari
kukandwa.
4. Kanda
unga wako kwenye bakuli, mpaka uone unaanza kulainika, waweza kukandia kwenye
flat surface ukiwa unauvuta vuta na kukanda vizuri mpaka uone unga haunati
kwenye mikono hapo unga wako utakuwa tayari umekandika.
5. Baada
ya kukanda pakaza mafuta kwenye bakuli
(waweza tumia sponge au brush) halafu weka dough kwenye bakuli yako kisha
funika na kitambaa safi. Acha utulie kwa dk 10 hivi.
6. Bada
ya dk 10, toa dough kwenye bakuli anza kukata miduara size ambayo utasukumia chapatti
(angalia picha)
7. Nyunyiza
unga kidogo sehemu ya kusukumia chapatti, sukuma maduara shape ya chapatti kisha,
pakaza mafuta upande mmoja wa chapatti then viringisha (angalia picha), hapa fanya
hvyo kwa maduara yote, kisha panga miviringo yako kwenye sinia ulilonyuniza
unga. Funika acha kwa dk 5.
8. Baada
ya dk 5, anza kuandaa kuchoma chapatti
9. Weka
flat skillet kwenye moto wa wastani, acha ipate moto, kisha nyunyiza unga
kidogo kwenye ubao wa chapati, sukuma chapati iwe na shape ya chapati kisha
weka kweye frying pan ya moto uanze kuchoma.
10. Acha
chapati ipate joto kisha geuza chapati upande wa pili ipate joto hapo ndo uweke
mafuta kidogo, halafu ugeuze geuze chapati hadi iive vizuri rangi ya golden
brown, toa chapati weka kwenye sahani au hot pot. Fanya hivyo kwa maduara yote
yalobaki mpaka umalize.
Chapati zitakua tayari waweza kula kama
dinner na maharage, roast ya nyama, au hata asubuhi kwa ajili ya kitafunwa.
NB: Ili upate chapate laini hutakiwi
kuwa na haraka kwenye kukanda, waweza tumia muda mrefu kwenye kukanda mpaka
dough iwe laini na isiyoshikana na mikono yako.
Maelekezo ya picha bonyeza hapa
Comments
Post a Comment