Skip to main content

Mapishi rahisi ya Cinnamon Rolls



Cinnamon rolls
Kwa mapishi rahisi angalia picha HAPA

Mahitaji

 Kwa kukandia 
-unga ngano 1/2 kg 
-hamira 2na 1/2 vijiko vya chai
-maziwa vuguvugu 1/4 kikombe
-Siagi 1/4 kikombe
-Chumvi 1/4 kijko chai
-Sukari 5 vijiko vya chakula  
-yai 1 kubwa 

Mahitaji ya kusukumia chapati.
-Mdalasini 3 vijiko vya chakula 
-Siagi iliyoyeyushwa  3 vijiko


Icing
-Cream cheese 1/2 kikombe
-Siagi vijiko 2 vya chakula
-Kijiko 1 cha vanilla extract
-Icing sugar kikombe 1
-Maziwa 2 vijiko

MAELEKEZO
-Chemsha maziwa yapate joto, weka hamira na sukari

-Changanya dry ingredients, kama unga na chumvi kidogo

-Mimina mix ya maziwa na hamira kwenye bakuli ya unga, tia yai, weka siagi,changanya na uanze kukanda, mpaka unga uache kunata kwenye mikono na iwe soft, weka mafuta kidogo kulainisha donge ulilokanda  huku ukizungusha.

-Unga uliokanda uache kwenye bakuli funikia sehemu yenye joto, kwa lisaa 1 na 1\2 au mpaka uumuke.

-Wakati  huo andaa mix ya sukari na mdalasini, yani mix sukari ya brown na mdalasini.

-Unga ukishaumuka kata maduara ya kutoshea kusukuma, nyunyiza unga kwenye ubao wa kusukumia ,sukuma kama chapati shape ya rectangle (angalia pichani), kisha yeyusha siagi pakaza na kisu kwa juu ya chapati uliosukuma, kisha nyunyiza mix ya sukari na cinnamon au mdalasini.

-Funga chapati yako kwa kuzungusha kisha anza kukata vipande (kuona picha ingia HAPA
 kisha andaa chombo cha kuokea kwa kupakaza siagi au weka baking paper ndio uanze kuvipanga vipande vyako kisha funika acha kwa dk 25 viumuke tena.

-Oka kwa 20 DK, pakaza ute wa yai rudisha kwenye moto, oka  kwa 20 dk au mpaka viwe brown, toa vitakua tayari.

Andaa icing wakati cinnamon rolls zipo jikoni
-Chukua cream cheese, maziwa, siagi na vanilla kisha changanya vizuri hadi iwe laini
-kisha chukua icing sugar mimina kidogo kidogo hadi iwe nzito

-Epua cinammon rolls, mwagia icing mix yako kwa juu  tayari kwa kula.


KUONA PICHA ZA CINNAMON ROLLS ZIKIWA TAYARI  ANGALIA PICHA HAPA

Comments

Popular posts from this blog

NJIA RAHISI YA KUTENGENEZA KEKI YA VANILLA

Jinsi ya Kupika Visheti/Vikokoto~Crunchy Visheti

Half Cake za maziwa