Skip to main content

Half Cake za maziwa



Viungo kwa Recipe ya Half keki
KWA MAELEKEZO YOTE YA PICHA UELEWE VIZURI TAFADHALI BONYEZA HAPA

  1. Unga ngano vikombe 2'
  2. Sukari 1/2 kikombe (kuongeza kulingana na upendeleo wako)
  3. Baking poda 2 ya kijiko chai
  4. Baking Soda 1/2 kijiko cha chai
  5. Margarine / siagi  3 kijiko chakula
  6. Maziwa 1/2 kikombe
  7. Mayai 2
  8. Vanilla kijiko 1
  9. Mbegu za  (Iliki) kijiko 1
  10. Mafuta kwa KUKAANGA
MAELEKEZO- kwa maelekezo yote ya picha tafadhali bonyeza hapa

  1. Changanya pamoja viungo vi kavu, (Unga, sukari, baking poda, baking soda, iliki) na umix ndani ya bakuli 
  2. Weka siagi na sugulia kwenye viungo vikavu
  3. Tengeneza shimo kati ya unga na ueke mayai na vanilla
  4. Weka maziwa kidogokidogo uanze kukanda unga wako, kwa dk5 hakikisha unakanda unakua unavutika, soft na haunati kwa mkono.
  5. Ukishakanda, chukua donge la duara ulilokanda weka kwenye bakuli kavu na safi, funikia kisha acha uumuke kwa dk40.
  6. Baadaya kuumuka, mwagia unga kwenye sehemu ya kusukumia, chukua dough(donge), lisukume kwa shape ya chapati
  7. Kata kata shape ya chapati, kwa urefu kutengeneza shape za half cake Angalia picha hapa step 7.Kisha pangilia vizuri half cake tayari kwa kukaanga.
  8. Weka mafuta kwenye frying pan, moto mdogo acha yachemke kisha dumbukiza halfcake mbichi, uanze kukaanga lakini usijaze karai yani visigusane
  9. Kanga upande mmoja hakikisha ipo brown nd.o ugeuze upande wa pili, acha ibadilik tango ndo utoe.
  10. ANGALIZO: kabla hujaweka batch nyingine ya half cake, epua mafuta kwanza yapoe kidogo kisha erudishe kwa moto wa kati ndio uongeze half cake nyingine.
  11. Weka kwenye chujio uliloweka tissue paper ili ichuje mafuta. 
  12. HALF CAKE TAYARI KWA KULIWA na Chai, maziwa, Juice au soda

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

NJIA RAHISI YA KUTENGENEZA KEKI YA VANILLA

Jinsi ya Kupika Visheti/Vikokoto~Crunchy Visheti